Thursday, August 23, 2012

Bibi Bomba 2012, ni Veronica aka Tukinao

Bi Vero aka Tukinao

Usiku wa jana mamia ya mashabiki  walipata kushuhudia Fainali ya lile shindano la kumtafuta Bibi Bomba Kupiatia TV ya watu Clouds Tv, na kupata kumshuhudia bibi Veronica aka Tukinao akiibuka kidedea na kuwabwaga mabibi waenzee saba ambao wote walikuwa washiriki wa mtanange huo, kufuatia ushindi huo wa kishindo wa kula nyingi dhidi ya wenzie saba waliobakia Bibi Vero alikjipatia shilingi milioni tano ikiwa kama zawadi ya ushindi        
Binafsi napenda kuwashukuru Clouds Tv kwa kutulete burudani nzuri kama hii na team nzima iliyoandaa shindano hilo, pili ni mashabiki wenzangu tuliompigia kura za kutosha bibi yetu bi Vero mpaka ameibuka na ushindi huo mnono
Ki ukweli alistahili kuwa mshindi kwani hata ukifatilia na kuangalia umri wake na mambo yake utagundua kuwa yeye ni bibi kuliko wale mabaibi wengine ukiondoa bi Nasra na Mwanaisha
Pia alikuwa ni burudani tosha kuanzia mwanzo wa kuwatafuta mpaka kwenye mjengo yani kila mtu aliyekuwa akitazama show ya bibi bomba alikuwa hawezi kujizuia kucheka  pale anapomsikia bi Vero akionge au akifanya mabo yake,
Viva bi Vero Bibi Bomba 2012
Tukinaooooooooooooooooooooooooooooo

No comments:

Post a Comment