Kwa wale wadada na kina mama wanaokwenda na wakati siku zote huwa hawapendi kuharibu hata kidogo haswa linapokuja lile swala la outing.
Mara nyingi huumiza vichwa vyao kutafuta nguo na viatu vizuri ili waonekane wenye kuvutia machoni mwa watu.
Na asikwambie mtu bwana siku zote thamani ya nguo huonekana pale tuu inapokuwa sambamba na kiatu kizuri kinachoendana na nguo husika,
Na hapo ndio utaona sifa zikimwagika dada au mama fuluni anavaa, anapendeza hakuna nguo inayomkataa,
Nimeshuhudia wanawake wengi katika sehemu mbali mbali wanavaa nguo nzuri lakini huko chini miguuni wamevaa viatu vya ajabu vinavyofuta kabisa thamani ya nguo alizovaa,
Napenda kuwashauri wanawake wote linapokuja swala la kuvaa ni vizuri ukatuliza akili utafuute kivazi kizuri kilichokuwa sambamba na kiatu kizuri ambacho kitakufanya uwe mwenye mvuto na kupendeza machoni mwa watu








No comments:
Post a Comment